Swali: Hakika mimi ni mwanamke ambaye nina mama aliyefariki kabla hajahiji Hijjah ya Uislamu. Ninataka nimtume mtu amhijie kutoka kwa mmoja wa watoto wangu. Je, inajuzu hilo au hapana?

Jibu: Ndiyo, ndiyo. Ikiwa amekufa mwanaume au mwanamke kabla ya kuhiji, basi wanamhijia jamaa zake, wasichana zake, mwanawe, mmoja wa jamaa zake, wengineo au wanamteua mtu amhijie katika watu wa kheri, basi yote haya ni mazuri. Hakika aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hilo: ”Hakika baba yangu amekufa na juu yake Hijjah ya Uislamu. Je, nimhijie?” Akasema: “Ndiyo, mhijie baba yako na mfanyie ´Umrah.”

Mwanamke mwingine alimuuliza akasema: ”Hakika baba yangu ni mzee mkubwa hawezi kukaa juu ya kipando. Je, nimhijie?” Akasema: “Mhijie baba yako.”

Wengine walimuuliza kuhusu ambaye juu yake kuna Hijjah au swawm, ambapo akawajibu kwamba wamhijie na wamfungie maiti wao.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3504/والدتي-توفيت-قبل-ان-تحج-فهل-لي-ان-اوكل-من-يحج-عنها
  • Imechapishwa: 28/08/2026