Swali: Nasaha inakaribia kupotea katika hii leo. Ni ipi sababu ya hilo kwa mtazamo wenu?
Jibu: Hakika bila shaka kunasihiana leo ni kidogo. Sababu zake ni udhaifu wa imani, uchache wa elimu, kushughulika kwa watu na mambo ya dunia na juhudi ya kila mmoja juu ya maslahi yake ya haraka – isipokuwa ambaye Allaah amemrehemu. Basi ilipodhoofika imani katika nyoyo mara nyingi, watu wakashughulika na mambo ya dunia, ikapungua elimu yao na uelewa wao katika dini, ndipo kukapungua nasah na kukapungua kuamrisha mema na kukataza maovu. Kila imani ilivyozidi kuwa na nguvu kwa watu, katika kijiji au katika mji na ikaongezeka elimu ndipo hupatikana kunasihiana na hupatikana kuamrisha mema na kukataza maovu kulingana na nguvu ya imani ya mji, katika kabila au katika kijiji. Kila ilivyozidi imani, elimu na ufahamu vikaongezeka, ukaongezeka uelewa katika dini na wakaongezeka watu wa kheri ndipo huongezeka ndani yao jambo hili. Kila ulivyozidi ususuwavu wa moyo, ujinga ukaongezeka, elimu ikapungua na huongezeka mashughuliko ya dunia ndipo hupungua nasaha na hupungua kuamrisha na kukataza – na Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3470/اسباب-ضعف-النصيحة-بين-المسلمين
- Imechapishwa: 28/08/2026
Swali: Nasaha inakaribia kupotea katika hii leo. Ni ipi sababu ya hilo kwa mtazamo wenu?
Jibu: Hakika bila shaka kunasihiana leo ni kidogo. Sababu zake ni udhaifu wa imani, uchache wa elimu, kushughulika kwa watu na mambo ya dunia na juhudi ya kila mmoja juu ya maslahi yake ya haraka – isipokuwa ambaye Allaah amemrehemu. Basi ilipodhoofika imani katika nyoyo mara nyingi, watu wakashughulika na mambo ya dunia, ikapungua elimu yao na uelewa wao katika dini, ndipo kukapungua nasah na kukapungua kuamrisha mema na kukataza maovu. Kila imani ilivyozidi kuwa na nguvu kwa watu, katika kijiji au katika mji na ikaongezeka elimu ndipo hupatikana kunasihiana na hupatikana kuamrisha mema na kukataza maovu kulingana na nguvu ya imani ya mji, katika kabila au katika kijiji. Kila ilivyozidi imani, elimu na ufahamu vikaongezeka, ukaongezeka uelewa katika dini na wakaongezeka watu wa kheri ndipo huongezeka ndani yao jambo hili. Kila ulivyozidi ususuwavu wa moyo, ujinga ukaongezeka, elimu ikapungua na huongezeka mashughuliko ya dunia ndipo hupungua nasaha na hupungua kuamrisha na kukataza – na Allaah ndiye Mwenye kutakwa msaada.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3470/اسباب-ضعف-النصيحة-بين-المسلمين
Imechapishwa: 28/08/2026
https://firqatunnajia.com/sababu-ya-kupungua-kunasihiana-kati-ya-watu/