Kutofautiana kwa waislamu katika mshahara katika kazi moja

Swali: Je, inajuzu kuwepo tofauti na kutofautiana baina ya waislamu katika malipo hali ya kuwa kazi ni sawa?

Jibu: Ndiyo, ndiyo inajuzu, inajuzu kuwepo tofauti. Watu wote hawako sawa. Mmoja anasema: mimi sifanyi kazi isipokuwa kwa kadhaa na mwingine anasema: mimi naridhia kufanya kwa kadhaa. Je, waambiwe hapana, lazima usawa na yule? Hapana. Ikiwa ana madereva wawili katika gari moja wanaloiendesha, huyu ana usiku na huyu ana mchana, au huyu ana saa na huyu ana saa, mmoja anasema: mimi si dereva kwako isipokuwa kwa kiasi fulani na mwingine anasema: mimi siridhii chini ya hicho, hakuna ubaya. Huyu anapewa 500 na huyu anapewa 400, hapana neno.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3461/اختلاف-الاجرة-بين-شخصين-مع-كون-العمل-متساويا
  • Imechapishwa: 28/08/2026