Kumruhusu mfanyakazi kufanya kazi binafsi kwa malipo ya kila mwezi

Swali: Je, inajuzu kwa mdhamini kumruhusu mfanyakazi wake afanye kazi kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe kulingana na ombi lake kwa kumpa mdhamini kiasi maalum cha pesa kila mwezi?

Jibu: Hapana, haifai. Hili halifai. Wajibu ni ikiwa hakuna budi, amlete kwa gharama yake yeye mwenyewe, kisha amtumie baada ya hapo katika anachotaka kwa masharti yaliyo baina yao, kila mwezi kwa kiasi fulani, kila mwezi kwa kiasi fulani. Amtumie katika aina ya kazi ambayo alimleta kwa ajili yake au katika kazi ambayo mfanyakazi anaridhia na mwenye kuajiri katika kazi yoyote iliyo halali Kishari´ah kwa njia ambayo imepangwa na nchi na imefafanuliwa na nchi kwa wale wanaoleta wafanyakazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3456/حكم-تاجير-الكفيل-مكفوله-الى-غيره-مقابل-مبلغ-شهري
  • Imechapishwa: 28/08/2026