Anaendelea kupokea pesa za udalali kila mwaka bila kufanya kazi yoyote

Swali: Katika baadhi ya watu wanawaleta wafanyakazi kwa idadi. Anamwekea mfanyakazi sharti alipe kwa mwaka 4,000, 5,000 ili akae hapo na kufanya kazi. Lakini yeye hafanyi kazi kwake kabisa. Je, kipato chake hiki ni halali au haramu?

Jibu: Hapana, haifai. Hili la yeye kuchukua pesa kwa dhamana yake na kuwaleta wafanyakazi. Hili ni katika sababu za shari kwa waislamu. Ni lazima kuleta wafanyakazi kufanyike kwa masharti yaliyodhibitiwa ambayo yamepangwa na serikali na kuratibiwa na serikali. Jambo hili limewasilishwa kwa baraza la wanazuoni wakubwa ambapo wakaamua hivyo na wakaandikia serikali kuhusu hilo, kwamba kuleta wafanyakazi kuwe kwa masharti yaliyodhibitiwa ambayo yamepangwa na serikali ili wasizidi waharibifu katika ardhi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3455/حكم-اشتراط-الكفيل-اموالا-على-مكفوليه-الذين-لا-يعملون-عنده
  • Imechapishwa: 28/08/2026