Swali: Je, mnaweza kutubainisha kwa undani ni nini kinachotupasa sisi kama waislamu kufanya kwa makafiri wanaofanya kazi pamoja nasi katika nchi zetu?
Jibu: Ndiyo, tunakushauri uwalinganie kwa Allaah, uwaongoze kwenye kheri na uwe mpole kwao. Usizidishe matusi, kejeli na ukali. Lazimiana na upole, hekima, maneno mazuri, kuwalingania kwa Allaah (´Azza wa Jall), uwe mwaminifu katika kazi yako, uwe bora zaidi yao na uwe mwenye nasaha zaidi kuliko wao katika kazi yako ili watu wakupendelee kuliko wao. Ikiwa waislamu watakuwa waaminifu, wakafanya kazi vizuri na wakaifanya kwa ubora, basi watu watawatanguliza juu ya makafiri. Lakini muislamu akifanya vibaya na akaghushi katika kazi yake, huenda wakamtanguliza kafiri juu yake ikiwa wataona uaminifu wa kafiri.
Kwa hiyo ni juu ya muislamu awe mwaminifu katika kazi yake, kwa maana asiwe mdanganyifu wala msaliti na ajitahidi katika kazi yake ili waislamu wampendelee juu ya maadui wa Allaah wanaoletwa kufanya kazi. Ikiwa uko pamoja nao, wanasihi, walinganie kwa Allaah, waelekeze kwenye kheri na ushirikiane nao katika mema, si katika mabaya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3453/واجب-المسلمين-تجاه-الكافرين-العاملين-في-بلادهم
- Imechapishwa: 28/08/2026
Swali: Je, mnaweza kutubainisha kwa undani ni nini kinachotupasa sisi kama waislamu kufanya kwa makafiri wanaofanya kazi pamoja nasi katika nchi zetu?
Jibu: Ndiyo, tunakushauri uwalinganie kwa Allaah, uwaongoze kwenye kheri na uwe mpole kwao. Usizidishe matusi, kejeli na ukali. Lazimiana na upole, hekima, maneno mazuri, kuwalingania kwa Allaah (´Azza wa Jall), uwe mwaminifu katika kazi yako, uwe bora zaidi yao na uwe mwenye nasaha zaidi kuliko wao katika kazi yako ili watu wakupendelee kuliko wao. Ikiwa waislamu watakuwa waaminifu, wakafanya kazi vizuri na wakaifanya kwa ubora, basi watu watawatanguliza juu ya makafiri. Lakini muislamu akifanya vibaya na akaghushi katika kazi yake, huenda wakamtanguliza kafiri juu yake ikiwa wataona uaminifu wa kafiri.
Kwa hiyo ni juu ya muislamu awe mwaminifu katika kazi yake, kwa maana asiwe mdanganyifu wala msaliti na ajitahidi katika kazi yake ili waislamu wampendelee juu ya maadui wa Allaah wanaoletwa kufanya kazi. Ikiwa uko pamoja nao, wanasihi, walinganie kwa Allaah, waelekeze kwenye kheri na ushirikiane nao katika mema, si katika mabaya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3453/واجب-المسلمين-تجاه-الكافرين-العاملين-في-بلادهم
Imechapishwa: 28/08/2026
https://firqatunnajia.com/kuwa-ni-mfano-mzuri-kwa-wale-wafanyakazi-makafiri-wanaoishi-nawe/