Mtu anapendwa na kuchukiwa kutokana na matendo yake

Swali: Je, mapenzi na chuki huwa kwa mtu mwenyewe au kwa matendo yake?

Jibu: Mapenzi na chuki huwa kwa matendo yake. Ikiwa ni muumini, anapendwa kwa imani yake, na ikiwa ni kafiri, anachukiwa kwa ukafiri wake. Si kwa sababu ya nasaba yake wala kwa sababu ya kuwa mweupe au mweusi, hapana. Anapendwa kwa imani na uchaji wake, hata kama ni mbaya zaidi kwa sura, na anachukiwa kwa ukafiri na upotofu wake, hata kama ni mzuri zaidi kwa sura au ana mali nyingi zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3446/الحب-والبغض-يكون-لعمل-الشخص-لا-لذاته
  • Imechapishwa: 27/08/2026