Wanandoa wote wanatakiwa kusaidiana katika kuboresha ujumba

Swali: Una nasaha yoyote kwa waume juu ya kutangamana na wake zao vizuri. Kwa sababu wengi wao wanatangamana na wake zao kwa njia ya kuonelea kuwa ni mfanyakazi. Ni upi umuhimu wa mwanamke katika jamii ya Uislamu?

Jibu: Ndio, mwanamke ndiye anayelazimika kumhudumia mume katika mipaka inayojulikana. Amhudumie katika mipaka inayojulikana. Vilevile ni juu ya mume asimtie uzito kwa kitu asichokiweza. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)

Wanandoa wote wanatakiwa kusaidizana kwa wema. Hapo ndipo kutapatikana kuishi kwa uzuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-28.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020