Wanandoa kugusa vitu baada ya jimaa kabla ya kuoga

Swali: Je, inafaa kwa wanandoa kugusa kitu chochote baada ya kufanya jimaa kabla ya kuoga? Wakigusa kitu chochote kinapatwa na najisi?

Jibu: Inafaa kwa mwanamke mwenye janaba kabla ya kuoga kugusa vitu ikiwa ni pamoja na nguo, masahani na vyungu. Ni mamoja ni mwanamme au mwanamke. Kwa sababu yeye sio najisi na wala havinajisiki vile alivyogusa. Vivyo hivyo mwanamke mwenye hedhi na damu ya uzazi hawawi najisi kwa damu zao. Bali miili yao na jasho lao ni visafi. Vivyo hivyo vile wanavyogusa kwa mikono yao. Ambacho ni najisi ni ile damu inayowatoka.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (4679)
  • Imechapishwa: 30/05/2022