Damu iliyorudi wakati wa usiku kwa mwanamke anayenyonyesha

Swali: Kuna mwanamke ananyonyesha na damu imekatika katika ile miezi mitatu ya mwanzo baada ya kuzaa kisha ikamrejelea aina fulani ya damu katika kipindi cha usiku. Lakini ilisimama katika kipindi cha mchana na hivyo akafunga kwa muda wa siku mbili. Baada ya hapo ikarudi damu kwa mara nyingine na ikaafikiana na ada yake ya mwezi. Je, inasihi swawm yake ya siku mbili hizi ambazo alitokwa na damu katika kipindi cha usiku zilizotangulia kwa kila siku moja?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ulivyotaja ya kwamba damu ilitoka katika kipindi cha usiku peke yake, basi funga yake ya siku mbili hizi ni sahihi na wala hakuna taathira ya kushuka damu katika kipindi cha usiku kwa siku zote mbili na wala damu hakuna taathira kwa damu kumrejelea juu ya kusihi kwa swawm ya siku mbili hizi.

Ibraahiym bin Muhammad Aalish-Shaykh

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Maaniy´

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/150) nr. (278)
  • Imechapishwa: 30/05/2022