Ameendelea kufanya ´ibaadah baada ya kumrejelea damu nyeusi

Swali: Ada yangu ya mwezi ilikatika na baadaye ikarudi baada ya siku kumi peke yake na ikaendelea kutoka kwa muda wa siku tatu mpaka nilipofanya matibabu na hivyo ikasimama baada yake na hapo ilikuwa katika Ramadhaan ya mwaka huu wa 1400 baada ya Hijrah. Lakini ndani ya kipindi cha siku hizi nne niliendelea na swawm yangu na kuswali hali ya kukusanya baada ya kutia twahara. Je, nilipe zile siku nne au inatosha swawm yangu iliyotangulia ijapo rangi ya damu katika kipindi cha siku zile nne ilikuwa nyeusi?

Jibu: Ni lazima kwako kufunga siku hizo nne. Kwa sababu swawm ambayo ulifunga kipindi ambacho ulikuwa na damu haikusihi kutokana na yale uliyotaja katika swali kwamba rangi ya damu katika kipindi cha zile siku nne ilikuwa nyeusi. Hii ni dalili ya kwamba ni damu ya hedhi.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (3550)
  • Imechapishwa: 30/05/2022