16. Si venginevyo Uislamu ni Qur-aan, Sunnah na Salaf

Dini si venginevyo ni Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall), mapokezi, Sunnah na masimulizi sahihi kutoka kwa wapokezi waaminifu ambapo mpokezi mmoja wa kwanza, mwaminifu na anayetambulika anasimulia kutoka kwa mwingine wa pili, mwaminifu na anayetambulika na wanasadikishana wao kwa wao mpaka yanafika kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanafunzi wa Maswahabah, wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah au wale maimamu wanaotambulika na wanaoigwa na kushikamana barabara na Sunnah, waliofungamana na mapokezi na ambao hawatambuliki kwa Bid´ah, hawatuhumiwi uwongo wala kwenda kinyume. Si wenye kujishughulisha na vipimo wala maoni yao wenyewe, kwa sababu vipimo katika dini ni batili. Maoni ya mtu mwenyewe ni mabaya zaidi. Watu wenye kuja na maoni yao wenyewe na vipimo katika dini ni  wazushi, wajinga na wapotofu. Isipokuwa ikiwa kama kitu hicho kinasapotiwa na upokezi kutoka kwa maimamu waaminifu waliotangulia hapo mwanzo; bora ni kutendea kazi mapokezi.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 01/06/2022