17. Jifunze ´Aqiydah ya Salaf na isomeshe

Ambaye atadai kuwa haonelei kufaa kuigiliza (التقليد) na wala hamwigilizi dini yake yeyote, basi huyo ni mzushi mtenda dhambi na adui wa Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), dini Yake, Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakika si venginevyo anachokusudia ni kubatilisha mapokezi, kuvuruga elimu, kuizima Sunnah na kufuata maoni yake mwenyewe, falsafa, Bid´ah na kwenda kinyume. Laana ya Allaah, Malaika na watu wote iwe juu ya mwenye kusema hivo!

Hizi ni miongoni mwa fikira mbaya kabisa za wazushi na zilizo karibu zaidi na upotofu na zenye kudharauliwa. Bali ni upotofu. Anadai kuwa yeye hamfuati yeyote ilihali amemwigiliza Abu Haniyfah, Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake. Ni adui yupi mkubwa wa dini ya Allaah kushinda yule ambaye anataka kuzima taa la Sunnah, anasambaratisha mapokezi na masimulizi na anadai kuwa hamfuati yeyote sambamba na hilo amewaigiliza wale tuliokutajia ambao ndio viongozi wa upotofu, vigogo wa Bid´ah na wakuu wa wenye kwenda kinyume? Ghadhabu za Allaah ziwe juu ya mwenye kusema hivo!

I´tiqaad na misemo hii niliyokutajia ni miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wanafuata mapokezi na kusimulia na kufikisha elimu. Tumechukua na kujifunza kutoka kwao na tumejifunza ´Aqiydah kutoka kwao. Walikuwa ni maimamu wenye kujulikana, waaminifu, waadilifu na wa kweli. Walikuwa ni wenye kuigilizwa na elimu yao ilitendewa kazi. Walikuwa hawana mambo ya Bid´ah. Si wenye kujigonga. Si wenye kuchanganya mambo. Hii vilevile ndio ´Aqiydah ya maimamu na wanazuoni wao kabla yao. Hivyo basi, hakikisha umeshikamana nayo, isome na ifunze.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 75-77
  • Imechapishwa: 01/06/2022