18. Hivi ndivo wanavoamini Murji-ah

Wazushi wenye majina bandia na majina ambayo hayaendani na majina ya watu wema, maimamu wala majina ya wanazuoni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni pamoja na:

Murji-ah. Ni wenye kudai kuwa imani ni maneno matupu pasi na matendo, kwamba imani ni yale maneno na matendo ni zile Shari´ah. Aidha imani ni kitu kimoja peke yake, watu hawashindani katika imani na kwamba imani yao ni moja kama imani ya Malaika na Manabii. Vilevile wanadai kuwa imani haizidi na wala haipungui na kwamba hakuna jambo la kufanya uvuaji katika imani. Ambaye atatamka kwa mdomo wake na asifanye matendo, basi huyo wanaona kuwa ni muumini wa kweli. Ukiongezea kwamba wanaona kuwa ni waumini mbele ya Allaah kwa marefu na mapana. Yote hii ni ´Aqiydah ya Murji-ah ambayo ndio ´Aqiydah mbaya kabisa na potevu zaidi.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 01/06/2022