19. Hivi ndivo wanavoamini Qadariyyah

Qadariyyah. Wanaona kuwa wanao uwezo, matakwa na ni waweza, kwamba wanamiliki kheri na shari juu ya nafsi zao, kudhuru na kunufaisha, kutii na kuasi, uongofu na upotofu. Wanaona kuwa watu ni wenye kutenda kwa utashi wao wenyewe pasi na Allaah kutangulia kulijua jambo hilo. ´Aqiydah yao inakumbushia ´Aqiydah ya waabudia moto na manaswara na ndio msingi wa uzandiki.

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Kirmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Sunnah, uk. 78
  • Imechapishwa: 01/06/2022