Swali: Katika mji wetu Amerika kuna baadhi ya wanamuziki wamesilimu na kuingia katika Uislamu. Wanafanya midhara kuwalingania vijana waingie katika Uislamu na waache kufuru. Lakini wakati mwingine wanataja katika mihadhara maasi na madhambi yao waliyokuwa wakifanya. Je, kitendo chao hichi ni sahihi?
Jibu: Hapana, si sahihi. Kuhusu kuwalingania kwao watu hili ni jambo zuri. Ama kutaja kwao maasi waliyofanya si sawa. Wasiyataje. Wayataje tu baina yao na nafsi zao ili watubie kwayo na kuomba msamaha kwayo. Kuhusiana na kuwatajia nayo watu pengine hata jambo hili likawaathiri wasikilizaji.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-16.mp3
- Imechapishwa: 19/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)