Pepo na Moto vinapatikana sasa?  

Swali: Je, Moto [an-Naar] unapatikana hivi sasa? Ni ipi hekima ya kupatikana kwake sasa? Vipi kuwaraddi wenye kupinga kuwepo kwake?

Jibu: Swali hili halina faida. Dalili zinaonyesha ya kwamba Moto upo sasa. Vilevile Pepo [al-Jannah] ipo. Yanayopitika duniani hivi sasa ni miongoni mwa alama zinatolea dalili kuonyesha kuwa upo. Ukali wa joto ni kutokana na athari ya Jahannam kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ

“Ulioandaliwa kwa makafiri.” (02:24)

“Ulioandaliwa”, hii inaonyesha kuwa upo. Hakusema:

“Wataandaliwa”, bali amesema:

أُعِدَّتْ

“Ulioandaliwa.”

Ni dalili inaonyesha kuwa upo.

Vilevile maiti anaadhibiwa kwenye kaburi lake. Hufunguliwa mlango wa Motoni. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa upo. Pamoja na kwamba hakuna faida kuingia sana kwa ndani katika mada hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-16.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020