Swali: Kuna mtu ameweka nadhiri ya kuacha kuvuta sigara wakati ambapo Allaah atamruzuku mke wake kushika mimba…

Jibu: Haijuzu kuchelewesha tawbah na kusema ntatubu huko mbeleni nikipata kadhaa. Hili halijuzu.

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ

“Hakika si venginevyo tawbah inayopokelewa na Allaah ni ya wale ambao wanafanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka.” (04:17)

Akimbilie kufanya tawbah. Haijuzu kuchelewesha tawbah.

Ukichelewesha tawbah una dhamana kuwa utabaki mpaka huo wakati uliyopanga? Hapana, huenda ukafa kabla ya wakati huo na hivyo ukafa juu ya dhambi. Harakisha kufanya tawbah!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-16.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020