Abul-Waliyd al-Faqiyh amesema: “Nilimsikia Ibn Rurayj akisema:

“Ni mara chache nimemuona msomi anayejishughulisha na falsafa akafaulu. Isitoshe atapitwa na elimu na hatofikia falsafa yenyewe.”

al-Haakim amesema: Nimemsikia Hassaan bin Muhammad akisema:

“Mwaka 303 tulikuwa katika kikao cha elimu cha Ibn Surayj ambapo akasimama mwanachuoni mmoja na kusema: “Pata bishara njema, ee hakimu! Kwani Allaah hutuma kila baada ya miaka mia mtu ambaye anaihuisha dini Yake.” Karne ya kwanza Allaah alimtuma ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz, karne ya pili akamtuma Muhammad bin Idriys ash-Shaafi´iy na karne ya tatu akakutuma wewe.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/202-203)
  • Imechapishwa: 09/11/2020