Ni chako ulichookota baada ya kukitangaza mwaka

Swali: Ni ipi hukumu ya kitu kilichomdondoka mtu endapo mtu atakiokota baada ya kutafuta mmiliki na asimpate yeyote?

Jibu: Ikiwa muokotaji ameokota mali hii kwa nia kwamba ataitangaza na kumtafuta mmiliki na akaitangaza mwaka mzima na asimpate mwenye nayo, basi inakuwa ni halali kwake na yenye kuingia ndani ya umiliki wake. Hivyo aitumie kama anavotaka.

Katikati ya mwaka au baada yake akija mwenye nayo na akamweleza kwa sifa zinazoendana nayo, basi ni lazima kwake kumkabidhi nayo.

Muulizaji: Akiila au akaitoa kisha akaja mwenye nayo na kumweleza nayo kwa sifa zinazoendana nayo?

Ibn ´Uthaymiyn: Kwanza haijuzu kuitumia kabla ya kukamilika mwaka. Bali ni lazima kwake kuihifadhi. Isipokuwa ikiwa ni kitu ambacho hakiwezi kuhifadhika mwaka mzima. Kama mfano wa baadhi ya vyakula ambavyo vinaharibika kwa kuviweka au kitu ambacho kukihifadhi kitapelekea matumizi makubwa na hivyo mtu akakiuza ili asalimike kutokamana na matumizi yake. Katika hali hii hakuna neno na ni lazima kwake kukitumia kama alivofanya. Kwa sababu ni katika ukamilifu wa shukurani. Lakini asikitumie mpaka ahakikishe kwanza. Akija mwenye nacho basi amweleze kwamba kitu hicho alichookota amekitumia kwa ajili ya kukihifadhi au kuepuka matumizi makubwa yanayopelekea kwa kukibakiza. Ama mwaka ukitumia basi yeye ndiye mmiliki wacho na akitumie atakavyo. Akija mwenye nacho basi ni lazima kwake kumrudishia mfano wake au waelewane.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (07) http://binothaimeen.net/content/6711
  • Imechapishwa: 09/11/2020