Swali: Nilisoma kitabu ulichoandika kiitwacho “al-Mutaqaa ar-Rasiyn” ambapo uliandika kuwa Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) madhehebu yake alikuwa ni Hanbaliy kwenye Fiqh na Salafiy kwenye ´Aqiydah. Nini maana yake?

Jibu: Ndio, hakuna ubaya. Ni Hanbaliy kwenye madhehebu na Salafiy kwenye ´Aqiydah. Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah ni Hanbaliy na ni Salafiy kwenye ´Aqiydah. Wanachuoni wote wenye kuhakiki wanafuata madhehebu manne kwenye Fiqh lakini ni Salafiyyuun kwenye ´Aqiydah. Kusema kuwa mwanachuoni hawezi kuwa mlinganizi maadamu anafuata moja katika madhehebu, hili ni kosa. Hakuna katazo mtu akafuata moja ya madhehebu ya Fiqh lakini katika ´Aqiydah akawa katika madhehebu ya Salaf.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com