Wanachuoni wa dini


Swali: Khofu iliyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si vyenginevyo wanaomcha Allaah miongoni mwa Wake ni wanazuoni.” (35:28)

Kunakusudiwa wanachuoni wa dini au inahusu pia wanachuoni wa elimu ya dunia ikiwa watatakasa nia zao ikawa kwa ajili ya Allaah pekee?

Jibu: Hapa wanakusudiwa wanachuoni wa Shari´ah.

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika si vyenginevyo wanaomcha Allaah miongoni mwa Wake ni wanazuoni.”

Ni wanachuoni wa Shari´ah. Ama wanachuoni wa dunia, wengi wao ni wakanamungu. Wengi wao ni wakanamungu na makafiri. Elimu hii ya dunia haikufanufaisha lolote. Kunaweza kupatikana katika wao yule ambaye ameongozwa na Allaah, akafaidika na akazingatia kuwa ni katika ishara za Allaah, lakini watu sampuli hii ni wachache. Watu sampuli hii ni wachache sana katika wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13252
  • Imechapishwa: 20/09/2020