Wanabiashara wanaokula kwa dhuluma mali za wenzao

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameharamisha kati yetu kuliana mali zetu pasina haki. Bila kujali ni kwa aina gani, ni mamoja ikiwa mtu ataichukua kwa kumpokonya mwenzake au kwa msemo mwingine akaichukua kwa kutumia mabavu, kwa kuiba, kwa ujanja, kwa khiyana, ghushi, kwa uongo na aina nyinginezo zote. Hili ni haramu kwake. Kujengea juu ya hili wale ambao wanawauzia watu kwa kufanya ghushi na khaswa wauzaji mboga, kila shilingi moja ya ziada anayopata katika thamani kwa kutumia ghushi ni haramu. Wale wanaotumia ghushi katika kununua au kuuza wanafanya maasi mawili:

1- Maasi ya kwanza ni kule kuwafanyia uadui ndugu zao waislamu kwa kuchukua pesa pasina haki.

2- Wanaguswa na kule Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kujitenga nao mbali. Ni ubaya uliyoje kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kujitenga nao mbali! Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kutufanyia ghushi, basi huyo si katika sisi.”[1]

[1]Muslim (101) na (102)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/119)
  • Imechapishwa: 28/02/2024