75. Kichenguzi cha saba cha swawm: Damu ya uzazi na hedhi

07 – Kutokwa na damu ya hedhi na ya uzazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu mwanamke:

“Je, si haswali wala hafungi pale anapopata hedhi?”

Swawm yake inaharibika pale atakapoona damu ya hedhi na nifasi. Ni mamoja mwanzoni mwa mchana au mwishoni mwake ijapo ni kitambo kidogo kabla ya kuzama kwa jua. Ikiwa atahisi kuhamahama kwa damu na isionekane isipokuwa baada ya kuzama kwa jua, basi swawm yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 102
  • Imechapishwa: 28/02/2024