Hanaabilah juu ya kujitolea viungo kumpa mgonjwa

Tambua kuwa kukata kiungo cha maiti ni kama kumkata ilihali yuko hai, kama ilivyokuja kutoka  kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]. Maiti anatakiwa kuheshimiwa. Haijuzu kuchukua chochote katika viungo vyake na wala kukata chohote kutoka kwenye viungo vyake. Kwa sababu ni amana. Atafufuliwa akiwa mkamilifu siku ya Qiyaamah.Mambo yakishakuwa ni hivo haijuzu kuchukua chohote kutoka kwake. Kwa ajili hii wanachuoni wa Hanaabilah (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa haijuzu kuchukua chochote katika viungo vya maiti hata kama ataacha anausia hilo. Hilo ni kwa sababu maiti ni mwenye kuheshimiwa. Kuvunja kiungo cha maiti ni kama kukivunja akiwa hai.

Tukichukua au kuvunja kiungo kutoka kwa maiti huko inakuwa ni kumtendea tendo la jinai nakumpetukia mipaka. Tunapata madhambi kwa kufanya hivo.

Maiti mwenyewe hana haki ya kutoa kitu katika viungo vyake. Kwa sababu viungo vyake ni amana alowekeshwa. Haijuzu amana hii akaitumia vibaya. Ndio maana Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ

”Wala msijiue.”[2]

[1] Abu Daawuud (3207).

[2] 4:29

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/117-118)