45. Je, ni wajibu kwa wanazuoni kuwabainishia vijana na watu wa kawaida khatari ya uvyamavyama, mifarakano na makundi?

Swali 45: Je, ni wajibu kwa wanazuoni kuwabainishia vijana na watu wa kaiwada khatari ya uvyamavyama, mifarakano na makundi?

Jibu: Ndio. Ni lazima kubainisha khatari ya uvyamavyama, migawanyiko na mifarakano. Haya yanatakiwa kufanywa ili watu wawe juu ya utambuzi. Watu wa kawaida wanadanganywa. Kuna watu wangapi wa kawaida wamepakwa mchanga wa machoni na baadhi ya makundi ambayo wanafikiria kuwa yako katika haki!

Kwa hivyo ni lazima kuwabainishia watu – wanafunzi na watu wa kawaida – khatari ya mapote na makundi. Kwa sababu wakinyamaza watu watasema:

”Wanazuoni walikuwa wakiyatambua haya na wakayanyamazia.”

Hivyo upotofu ukaingia kupitia mlango huu. Wakati kunapojitokeza mambo kama haya basi ni lazima kubainisha. Watu wa kawaida wako katika khatari kubwa zaidi kuliko ilivyo kwa wanafunzi. Kwa sababu pindi watu wa kawaida wanapoona wanazuoni wamenyamaza, wakadhani kuwa hayo yanayoendelea ndio sahihi na ndio haki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 131
  • Imechapishwa: 28/02/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy