Swali 44: Je, kuna tofauti kati ya ´Aqiydah na mfumo?

Jibu: Mfumo imeenea zaidi kuliko ´Aqiydah. Mfumo inakuwa katika ´Aqiydah, tabia, maadili, miamala na katika maisha mazima ya muislamu. Kila hatua inayochukuliwa na muislamu inaitwa mfumo.

Kuhusu ´Aqiydah, kunakusudiwa msingi wa imani, maana ya shahaadah na yale yanayopelekea huko. Hiyo ndio ´Aqiydah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 130-131
  • Imechapishwa: 28/02/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy