Swali: Kuna mtu alimkopa mwenzake kiwango fulani cha pesa kisha baada ya hapo wakati wa kulipa akamzidishia pesa kidogo.

Ibn Baaz: Pasi na kumuwekea sharti?

Muulizaji: Pasi na kumuwekea sharti.

Jibu: Hapana vibaya. Wabora wa watu ni wale wabora wao katika kulipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikopesha 30 akirudisha mpaka 60. Ikiwa hakushurutishiwa hapo awali hapana vibaya. Wabora wa watu ni wale wabora wao katika kulipa.

Swali: Ni kitu kisichoingia ndani ya Hadiyth inayosema:

“Mkopo wowote ambao unapelekea katika manufaa basi ni ribaa?”

Jibu: Hapana. Hapo ni pale ambapo mtu atawekewa sharti awali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22128/حكم-الزيادة-في-رد-القرض-دون-شرط
  • Imechapishwa: 31/10/2022