Imamu kubaki ameelekea Qiblah baada ya Fajr na Maghrib

Swali: Baada ya Fajr na Maghrib imamu anatakiwa kubaki hali ya kuelekea Qiblah mpaka alete Tahliyl?

Jibu: Hapana, ni kosa. Sunnah ni yeye kuwaelekea waswaliji anaposema:

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Awageukia maamuma. Hii ndio Sunnah.

Swali: Je, kuna makatazo ya kuelekea Qiblah?

Jibu: Hapana, hichi ndicho kilikuwa kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Swalini kama mlivyoniona ninaswali.”

Alikuwa akileta Maghfirah mara tatu husema:

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

kisha anawageukia watu. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyesema:

“Mtume alikuwa akigeuka wakati anapomaliza kusema:

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22137/هل-يهلل-الامام-الى-القبلة-في-الفجر-والمغرب
  • Imechapishwa: 31/10/2022