´Abdullaah bin Unays amepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Allaah atawafufua viumbe siku ya Qiyaamah wakiwa uchi, peku, hawakutahiriwa na bila ya kitu na atawanadi kwa sauti watayomsikia walio mbali kama wanavyomsikia walio karibu: “Mimi ndiye mfalme! Mimi ndiye Mwenye kuhukumu!””

Ameipokea al-Bukhaariy kwa cheni ya wapokezi pungufu kwa njia ya kutokukata (التمريض). Mtunzi wa “al-Fath” amesema: “Ameipokea mtunzi wa kitabu katika “Adab-ul-Mufrad“, Ahmad na Abu Ya´laa katika “Musnad” zake mbili na amezitajia njia mbili zingine. Maneno ya Allaah aina yake ni ya kale milele (قديمة النوع), na yanazuka kutegemea na matukio (حادثة الآحاد). Maana ya (قديمة النوع) ni kuwa Allaah alikuwa na hajaacha kuwa mwenye kuzungumza. Kwa msemo mwingine ni kwamba maneno hayakuzuka kutoka Kwake baada ya kutokuwepo kwake. Maana ya (حادثة الآحاد) ni kuwa maneno Yake fulani ni yenye kuzuka kwa sababu yamefungamana na matakwa Yake pale anapotaka. Anazungumza kwa akitakacho na pale anapotaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 31/10/2022