42. Ashaa´irah kuhusu maneno ya Allaah na majibu juu yao

2 – Ashaa´irah. Wanaona kuwa maneno ya Allaah ni kitu kilichosimama peke yake na hakifungamani na matakwa Yake. Herufi hizi na sauti zinazosikiwa ni vitu vilivyoumbwa ili vielezee juu ya ile maana iliyosimama katika nafsi ya Allaah. Tunawaraddi ifuatavyo:

1 – Ni kitu kinaenda kinyume na maafikiano ya Salaf.

2 – Ni kitu kinaenda kinyume na dalili. Kwa sababu yanafahamisha kuwa maneno ya Allaah ni yenye kusikiwa na hakuna kinachosikiwa isipokuwa ni ile sauti. Kinachosikiwa sio ile maana iliyosimama kwenye nafsi.

3 – Ni kitu kinaenda kinyume na kilichozoeleka. Maneno yaliyozoeleka ni yale yanayotamkwa na mzungumzaji na si yale anayoyadhamiria nafsini mwake.

Dalili ya kuwa maneno ya Allaah ni kwa herufi ni maneno Yake (Ta´ala):

يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا رَبُّكَ

“Ee Muusa! Hakika Mimi ni Mola wako.”[1]

Maneno haya ya Allaah ni kwa herufi.

Dalili ya kwamba ni kwa sauti ni maneno Yake (Ta´ala):

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.”[2]

Kuitwa hakukuwi isipokuwa kwa sauti.

[1] 20:11-12

[2] 19:52

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 73
  • Imechapishwa: 31/10/2022