41. Jahmiyyah kuhusu maneno ya Allaah na majibu juu yao

Wapinzani wa Ahl-us-Sunnah kuhusu maneno ya Allaah (Ta´ala).

Yako mapote yaliyokwenda kombo na Ahl-us-Sunnah. Tutataja miongoni mwayo mapote mawili:

1 – Jahmiyyah. Wanaona kuwa maneno sio katika sifa za Allaah. Hakika si venginevyo ni kiumbe miongoni mwa viumbe vya Allaah. Allaah anayaumba angani au katika mahali yanaposikika. Allaah ameyaegemeza Kwake kama kiumbe au kwa njia ya kuyatukuza. Ni kama mfano wa ngamia wa Allaah au nyumba ya Allaah. Tunawaraddi ifuatavyo:

1 – Ni kitu kinapingana na maafikiano ya Salaf.

2 – Kinaenda kinyume na akili. Maneno ni sifa ya yule mzungumzaji na sio kitu kinachosimama peke yake kilichotengana na yule mzungumzaji.

3 – Muusa alimsikia Allaah akisema:

إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي

”Hakika mimi ni Allaah, hakuna mungu wa haki isipokuwa Yeye, basi niabudu.”

Haiwezekani kabisa akasema hivo mwingine isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 31/10/2022