Swali: Kuna mtu aliniuliza kuhusu hukumu ya kujitoa manii na nikawa nimemjibu kuwa nijuavyo ni kwamba ni haramu. Akaniomba dalili na nikawa sijui. Ni ipi dalili?

Jibu:

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ

“Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.” (23:05-06)

Haikuhalalishwa kutumia tupu isipokuwa kwa mke au yule aliyemilikiwa na mikono ya kiume.

Yule mwenye kutoa manii kwa kutumia mkono, huyu ameufanya mkono wake kuwa ndio mke wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020