Swali: Kuna mtu ameoa na hajataka kupata watoto kwa sasa. Je, inajuzu kwake kufanya al-´Azl [kuchopoa kabla ya kumwaga] kwa mkewe?

Jibu: Haijuzu ikiwa kama anachukia watoto. Ama ikiwa anafanya hili kwa sababu, pengine mwanamke ni mgonjwa na hawezi kushika mimba kutokana na maradhi yake, ni sawa kufanya al-´Azl kwa sababu inayoruhusiwa. Ama kuchukia watoto ni jambo lisilojuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (66) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-04-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020