Walinganizi sampuli hii ndio hutokea fitina kati yao

Swali: Tufanye nini wakati ambapo kunatokea fitina kati ya wanachuoni wa Ah-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Hakutotokea fitina kati ya wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wanachuoni wanaojulikana hakutatokea fitina kati yao. Fitina hutokea kati ya wale wenye kujifanya kuwa wanachuoni au wale wenye kuanza kutafuta elimu. Watu sampuli hii ndio hutokea fitina kati yao kwa sababu ya uchache wa elimu yao. Ama kuhusu wanachuoni waliobobea hakutokea fitina kati yao na himdi zote ni za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (77) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-11-19.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020