Swali: Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotaja wale watu 70.000 ambao wataingia Peponi pasi na hesabu wala adhabu akataja miongoni mwao ya kwamba ni wale wasioomba kufanyiwa matabano. Je, inahusiana na matibabu yote? Vipi tutaoanisha na Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aombe kufanyiwa matabano dhidi ya kijicho? Je, tumwamrisha mtu ambaye amepatwa na kijicho kufanya matabano au tumwelekeze kufanya subira?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu wale 70.000:
“Ni wale ambao hawaombi kufanyiwa matabano… “[1]
Kwa maana ya kwamba hawawaombi wengine wawafanyie matabano. Hata hivyo ameamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kujitibisha na akasema:
“Allaah hakuteremsha maradhi yoyote isipokuwa aliteremsha pia dawa; ameijua yule mwenye kuijua na ameijahili yule mwenye kuijahili.”[2]
Tofauti kati ya hayo mawili ni kwa njia mbili:
1 – Mtu anafungamana zaidi na matabano kuliko anavyofungamana na matibabu. Allaah akijaalia kumponya mgonjwa huyu kupitia matabano haya, basi kunakuwa na mafungamano ya kiroho baina yao na pengine akatahiniwa naye na akaanza kusema kuwa mtu huyo ni katika mawalii wa Allaah na mfano wa hayo. Pengine jambo likapea zaidi na kwenda katika shirki. Kwa ajili hiyo katika Hadiyth hiyohiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“… na wanamtegemea Mola wao.”
2 – Kuna uwezekano mtu akamuomba ambaye hastahiki kufanya matabano kwa sababu mtu huyu anatibu kwa vitu yenye kuhisiwa. Mgonjwa huyu asipone kwa matabano hayo kwa sababu hayakusuniwa lakini hata hivyo akapona wakati wa kufanyiwa matabano. Matokeo yake watu wakatahiniwa na mtu huyu na wakadhani kuwa ni miongoni mwa watu ambao yanaitakiwi maombi yao na ambao kunatafutwa baraka kwa kisomo chake. Ukweli wa mambo siyo hivyo. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Ni wale ambao hawaombi kufanyiwa matabano… “
Hakusema hawajitibishi. Kwa msemo mwingine kujitibisha ni jambo linalotakikana tofauti na kuomba kufanyiwa matabano ni bora kuepuka jambo hilo. Lakini iwapo mtu mwenyewe ndiye ambaye atajitolea na akufanyia matabano na usimzuie kufanya hivo, hakumzuilii mtu kuingia ndani ya Hadiyth hii kwa sababu si wewe uliyeomba kufanyiwa matabano. Vivyo hivyo endapo utajitolea kumfanyia matabano ndugu yako umemfanyia jambo jema. Wala hutoki nje ya hawa 70.000. Kwa ajili hiyo ziada ilioko kwa Muslim isemayo:
“Ni wale ambao hawafanyi matabano… “
ni dhaifu na sio Swahiyh. Tamko la sawa ni lile lisemalo:

Mwanachuoni anafanya matabano kwa sababu ni msomi na kwa ajili hiyo anatakiwa kutabana kwa sababu ananufaisha kwa idhini ya Allaah, ni kama daktari anayemtibu mgonjwa.
Kuhusiana na kwamba mtu ambaye amepatwa na kijicho, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameelekeza njia ya kutibu kutokana na kijicho. Alimwamrisha yule bwana ambaye alimsibu kijicho mmoja katika Maswahabah aoge na atawadhe, kisha baada ya hapo yachukuliwe maji yake na kumwagiliwa yule mgonjwa ili aweze kupona[3].
[1] al-Bukhaariy (5705) na Muslim (220).
[2] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (3/75). Swahiyh kwa mujibu wa Ibn ´Abdil-Barr katika ”at-Tamhiyd” (5/283).
[3] Maalik (2/938) na Abu Daawuud (3880).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/35-37)
- Imechapishwa: 06/07/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/35-37)
Imechapishwa: 06/07/2026
https://firqatunnajia.com/wale-wasiowaomba-watu-wawafanyie-matabano/