Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kisha, wakati vitabu vya kirumi na kigiriki vilipofanyiwa tarjama kwa kiarabu katika miaka ya 200 ndipo shari ikawa kubwa zaidi. Ukiongezea na ule upotofu ambao shaytwaan alikuwa amewadanganya watu wapotevu.
MAELEZO
Anataka kubainisha ni lini upotofu uliingia kwa waislamu; ulikuwa pale vitabu vya kirumi vilipotafsiriwa kwa kiarabu katika zama za al-Ma’muun. Navyo vilikuwa vina falsafa, elimu ya maneno na mantiki. Wanaviita kuwa ndio hoja na dalili, kwa sababu hawakuwa na chochote katika wahy, bali walikuwa wakitegemea akili zao na yale wanayosema waliotangulia wao na wakiyarithishana. Uislamu ulikuwa salama kutokana na vitabu hivi. Waislamu walikuwa wakitosheka na Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf katika Maswahabah na wanafunzi wao. Hakukutokea upungufu kwa waislamu kwa sababu vitabu hivi havikuwa vimeingia kwao, wala havikuwa katika lugha yao na hawakuvijua, kwa sababu vilikuwa ni vitabu vya kigeni. Walikuwa wamejitosheleza kwa Qur-aan na Sunnah.
Kisha katika zama za al-Ma’muun al-´Abbaasiy, alikuwa amevutiwa mno na vitabu hivyo vya kigeni kwa sababu ya watu wa karibu naye miongoni mwa Mu´tazilah ambao walikuwa wakitegemea elimu ya mantiki. Yeye alichukua ukhaliyfah baada ya ndugu yake al-Amiyn. Haruun ar-Rashiyd (Rahimahu Allaah) alipofariki alimrithi mwanawe al-Amiyn. Kisha al-Ma’muun alimwasi, akavunja utiifu dhidi yake na hatimaye ukhaliyfah ukaishia kwa al-Ma’muun. Alikuwa mtu mwenye akili na nguvu, lakini aliwafanya mawaziri watu wa upotovu katika Mu´tazilah, kama Bishr al-Mariysiy na Ibn Abiy Du-aad. Alikuwa akielemea kwa hawa na hivyo wakamuathiri katika ´Aqiydah yake na wakamvutia kwenye vitabu hivi na wakavisifu mbele yake. Alikuwa amevutiwa sana na utamaduni na elimu. Hivyo akaathirika navyo. Hivi ndivyo mtu huathirika na vikao vyake na watu wake wa karibu ikiwa ni watu wa shari. Hivyo akaikubali ´Aqiydah ya Mu´tazilah na ´Aqiydah ya kwamba Qur-aan ni kiumbe. Akataka kuwalazimisha watu kusema kwamba Qur-aan ni kiumbe. Akawafanyia watu mtihani mkali sana. Akaua aliowaua na akawapiga aliowapiga. Akampiga Imaam Ahmad na akamfunga gerezani. Lakini Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) alisimama imara, akathibiti na akavumilia kupigwa, kufungwa na kudhalilishwa. al-Ma’muun aliwadhulumu maimamu. Yote haya yalikuwa kwa sababu ya marafiki wabaya. Vinginevyo yeye asili yake hakuwa miongoni mwao, lakini walimuathiri. Matokeo yake akaikubali ´Aqiydah yao na akadhani kuwa ni haki na kwamba ni hoja na dalili. Hivyo ´Aqiydah hii ikamdanganya. Lakini Allaah Akamsimamisha Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) naye akathibiti. Watu wakamfuata, akavumilia kifungo, kupigwa na mtihani.
Kisha al-Ma’muun alipokufa, alimrithi ndugu yake al-Mu´taswim. Naye akaendelea juu ya njia ileile ya al-Ma’muun. Akaendeleza mtihani, akampiga Imaam Ahmad na akamfunga gerezani. Kisha zikaja zama za al-Waathiq baada ya al-Mu´taswim. Makhaliyfah watatu wote walikuwa juu ya mwenendo huu. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) alikuwa imara habadiliki. Watu walikuwa wakimtazama aone atasema nini. Walikuwa wakimpiga ili aseme kwamba Qur-aan ni kiumbe, ilihali yeye alikuwa akisema:
“Nileteeni dalili kutoka katika Kitabu cha Allaah au kutoka katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Qur-aan imeteremshwa, si yenye kuumbwa.”
Kisha Allaah akaleta faraja. al-Waathiq akaaga dunia. Inasemekana kwamba alirudi katika haki mwishoni mwa siku zake. Allaah ndiye Mjuzi zaidi. Lakini alikufa. Akaja baada yake al-Mutawakkil, mwana wa al-Mu´taswim. Huyo akainusuru Sunnah, akaondoa mtihani na akamuheshimu Imaam Ahmad. Hapo ndipo haki ikashinda kwa mkono wa al-Mutawakkil. Akamkaribisha Imaam Ahmad, akamuheshimu na akamsaidia. Hivyo mtihani ukaondoka na himdi zote njema ni za Allaah. Watu wa haki wakashinda na watu wa batili wakaangamia.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 181-184
- Imechapishwa: 06/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 181-184
Imechapishwa: 06/07/2026
https://firqatunnajia.com/116-namna-hii-ndio-marafiki-wabaya-humuathiri-mtu/