Swali: Mwanamke ameolewa na kupokea mahari yake. Mahari yakabaki miaka miwili pasi na kuyagusa. Je, ayatolee zakaah? Hivi sasa familia yake wanafanya biashara kwayo. Je, mahari hayo yanapaswa kutolewa zakaah kwa kipindi chote hicho au yatatolewa zakaah kwa kile kipindi tu ambacho yalianza kufanyiwa biashara?
Jibu: Mtu analazimika kuzitolea pesa zakaah pale tu zinapofikisha kile kiwango cha wajibu kutoa zakaah. Uwezekano mwingine ni pale anapokuwa na bidhaa za biasharaa zinazokamilisha pesa zake. Kwa sababu pesa yenyewe kama yenyewe inawajibika kutolewa zakaah na kwa ajili hiyo haishurutishwi kuifanyia biashara, matumizi, ndoa, kujenga nyumba ya lazima, kukodisha na mfano wa hayo ili eti itolewe zakaah. Pesa kama hiyo inatolewa zakaah kwa hali yoyote ile. Kwa ajili hiyo ambaye amehifadhi pesa ndani ya benki anatakiwa kuitolea zakaah kila mwaka. Ni mamoja pesa hizo amezinuilia kufanya nazo biashara au hakufanya hivo. Kwa hiyo ni lazima kwa mwanamke huyo kuyatolea zakaah mahari yake aliyoyahifadhi kwa muda wa miaka miwili bila ya kuyafanya biashara na ayatolee zakaah pia kwa kipindi cha ile miaka mingine ambayo aliyafanyia biashara.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/191-192)
- Imechapishwa: 06/07/2026
Swali: Mwanamke ameolewa na kupokea mahari yake. Mahari yakabaki miaka miwili pasi na kuyagusa. Je, ayatolee zakaah? Hivi sasa familia yake wanafanya biashara kwayo. Je, mahari hayo yanapaswa kutolewa zakaah kwa kipindi chote hicho au yatatolewa zakaah kwa kile kipindi tu ambacho yalianza kufanyiwa biashara?
Jibu: Mtu analazimika kuzitolea pesa zakaah pale tu zinapofikisha kile kiwango cha wajibu kutoa zakaah. Uwezekano mwingine ni pale anapokuwa na bidhaa za biasharaa zinazokamilisha pesa zake. Kwa sababu pesa yenyewe kama yenyewe inawajibika kutolewa zakaah na kwa ajili hiyo haishurutishwi kuifanyia biashara, matumizi, ndoa, kujenga nyumba ya lazima, kukodisha na mfano wa hayo ili eti itolewe zakaah. Pesa kama hiyo inatolewa zakaah kwa hali yoyote ile. Kwa ajili hiyo ambaye amehifadhi pesa ndani ya benki anatakiwa kuitolea zakaah kila mwaka. Ni mamoja pesa hizo amezinuilia kufanya nazo biashara au hakufanya hivo. Kwa hiyo ni lazima kwa mwanamke huyo kuyatolea zakaah mahari yake aliyoyahifadhi kwa muda wa miaka miwili bila ya kuyafanya biashara na ayatolee zakaah pia kwa kipindi cha ile miaka mingine ambayo aliyafanyia biashara.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/191-192)
Imechapishwa: 06/07/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-ya-mahari/