Wakusudiwa wa ”Rifqan Ahl-as-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah” sio Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Kunaenezwa tetesi kati ya baadhi ya vijana kwamba Shaykh ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad amejirejea kusifu kwake kitabu  ”Madaarik-un-Nadhwar” cha Shaykh ´Abdul-Maalik na kwamba dalili ya kujirejea kwake ni kitabu chake kilichochapishwa ”Rifqan Ahl-as-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah”. Unayaraddi vipi maneno haya?

Jibu: Mosi ni kwamba kitabu ”Madaarik-un-Nadhwar” nimekisoma mara mbili. Nimeulizwa mara nyingi kama nimesoma sehemu tu ya kitabu hicho au nimekisoma chote. Ndipo nikasema kuwa nimekisoma mara mbili kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake. Mara ya kwanza nilipoulizwa sikuwa nimeulizwa kuandika kitu juu yake. Nikakisoma. Wakati nilipokisoma nikamwambia mtunzi kwamba nimekisoma na kwamba kina faida. Akaniomba kukiandikia dibaji. Nikamwambia kwamba nitakisoma mara ya pili. Ndipo nikakisoma kuanzia mwanzo hadi mwisho. Nikasahihisha baadhi ya maeneo ambayo niliona hayako sawa. Kwa hiyo kitabu nimekisoma chote kuanzia mwanzo hadi mwisho. Nimezindua baadhi ya vitu na nikawataja baadhi ya watu na sijajirejea juu ya chochote nilichoandika.

Kitabu changu nilichoandika mara ya mwisho ”Rifqan Ahl-as-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah”  hakina mafungamano yoyote na wale niliyowataja ndani ya ”Madaarik-un-Nadhwar”. Wale niliyowataja ndani ya ”Madaarik-un-Nadhwar” hawana uhusiano wowote na ”Rifqan Ahl-as-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah”.  Kitabu changu ”Rifqan Ahl-as-Sunnah bi Ahl-is-Sunnah” sikuwakusudia al-Ikhwaan al-Muslimuun, watu waliyoathirika na Sayyid Qutwub na wanaharakati wengine, watu waliyoathirika na mambo ya kisasa (Fiqh-ul-Waaqiy´), watu wanaowasema vibaya watawala na kuwakimbiza watu mbali na wanazuoni. Kitabu hakiwahusu watu hawa si kwa karibu wala kwa mbali. Kitabu hiki kinawalenga Ahl-us-Sunnah peke yao na ambao wanalazimiana na njia  ya Ahl-us-Sunnah ambapo wakaanza kujeruhiana, kukatana na kusemana vibaya kwa sababu ya mambo ya tanzu yanayotokea kati yao.

Kitabu hiki hakiwahusu mapote haya na makundi potofu yaliyoacha mfumo na njia ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kinawahusu watu katika Ahl-us-Sunnah ambao wanajishughulisha kujeruhi, kukata, kukaripia na kuwatahadharisha wengine katika Ahl-us-Sunnah kwa sababu ya makosa.

Kunapotokea tofauti kati ya watu wawili, basi Ahl-us-Sunnah wanagawanyika makundi mawili. Kundi moja linamsapoti huyu na lingine linamsapoti mwingine. Baada ya hapo kunatokea kukatana na kususana kati Ahl-us-Sunnah kila mahali kutokana na sababu ya tofauti hii. Hili ni janga na mtihani mkubwa. Namaanisha Ahl-us-Sunnah kukatana na kususana kwa sababu ya tofauti kati ya mtu na mwingine. Ukishika msimamo fulani, unasalimika. Ikiwa huna msimamo wowote unakuwa mzushi. Baada ya hapo kunatokea kukatana na matokeo yake Ahl-us-Sunnah wanagawanyika katika mgawanyiko huu khatari. Hili ndio lengo la kitabu hiki.

Inatambulika kuwa kitabu hiki hakiwapendezi wanaharakati. Kwa sababu wanaharakati wanachotaka ni kuwaona Ahl-us-Sunnah wakijishughulisha hawa kwa wengine ili Ahl-us-Sunnah wapate kusalimika nao. Hili hutokea pindi Ahl-us-Sunnah wanashughulika hawa kwa wengine. Kitabu hiki kinalingania Ahl-us-Sunnah kuungana na wawe na urafiki kati yao na kunasihiana. Hili ndio lengo la kitabu hiki.

Kuhusu harakati na watu wanaoenda kinyume na njia ya Ahl-us-Sunnah, wanafurahishwa na tofauti hii. Kwa sababu Ahl-us-Sunnah wakijishughulisha hawa kwa hawa, basi wao wanapata kusalimika na vita vinakuwa kati ya Ahl-us-Sunnah. Hili ndilo wanalolitaka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=RrYS3ROluzM
  • Imechapishwa: 06/11/2022