Swali: Unasemaje kuhusu al-Qaradhwaawiy kuhusu fatwa potofu anazotoa Qatar na amewazungumzia vibaya baadhi ya ndugu Salafiyyuun Qatar na akasema kuhusu kupunguza nguo na kufuga ndevu kwamba ni mambo yanayopendeza tu ambayo haitakiwi kwa mtu kujishughulisha nayo?

Jibu: al-Qaradhwaawiy ameacha sehemu ya dini na kuna khatari akaiacha yote. Ni Hizbiy. Ana kitabu ambacho anajuzisha kuwepo kwa makundi mengi katika Uislamu. Nimekwishazungumza sana mbali na kanda hii ya kwamba haijuzu kuwepo kwa makundi mengi katika Uislamu na kwamba waislamu ni kundi moja tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa Allaah uko pamoja na mkusanyiko.”

Hakusema “mikusanyiko”. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ikiwa hakuna mkusanyiko wala kiongozi basi yaepuke makundi yote ijapo utahitaji kung´ata shina la mti.”

“Yeyote atakayefarikiana na mkusanyiko ambapo akafa, basi amekufa kifo cha kipindi kabla ya kuja Uislamu.”

Allaah (Subhaanah) amesema:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

”Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja wala msifarikiane.” (03:103)

وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ

”Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja Nami ni Mola wenu. Hivyo nicheni.” (23:52)

Ni lazima kwa waislamu kuwa kundi moja. Nimeshazungumza sana kwenye kanda nyingi ya kwamba makundi haya yamezuliwa isipokuwa lile kundi linalofuata Qur-aan na Sunnah. Tunataraji tuko katika kundi hilo linalofuata Qur-aan na Sunnah.

Kuhusu al-Qaradhwaawiy, mtu hatakiwi kuzingatia fatwa zake, mawaidha yake wala ulinganizi wake. Nimeambiwa na baadhi ya ndugu wa Algeria ya kwamba serikali ya Algeria wamemuomba al-Qaradhwaawiy na al-Ghazaaliy kuja kuwapotosha vijana. Kwa sababu wapo baadhi ya wasichana walikuwa wanakataa kusoma shule za mchanganyiko. Hivyo al-Qaradhwaawiy akasema kuwa yeye yuko na wasichana wawili ambapo mmoja anasoma nje na mwingine anasoma Ghuba. Kwa hivyo ni mtu Hizbiy ambaye hatakiwi kufuatwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Naswaa’ih wa Fadhwaa’ih, uk. 280-281
  • Imechapishwa: 06/11/2022