Matakwa ya Allaah yamegawanyika sampuli mbili:

1 – Matakwa ya kilimwengu.

2 – Matakwa ya kidini.

Matakwa ya kilimwengu ni yale yenye maana ya kutaka. Kama vile maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا

“Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza, humfungulia kifua chake kwa Uislamu na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye uzito.”[1]

Matakwa ya kidini ni yale yenye maana ya kupenda. Amesema (Ta´ala):

وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ

“Allaah anataka kukusameheni.”[2]

Tofauti kati yao ni kwamba matakwa ya kilimwengu ni yale ambayo ni lazima kitokee kile kilichokadiriwa na hailazimishi Allaah kukipenda kilichotokea. Kuhusu makadirio ya kidini ni lazima yawe yanapendwa na Allaah na hailazimishi yatokee.

[1] 06:125

[2] 04:27

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 97
  • Imechapishwa: 06/11/2022