54. Mtazamo wa Qadariyyah juu ya makadirio ya Allaah

2 – Qadariyyah. Wanasema kuwa mja ni mwenye kujitosheleza kwa matendo yake na kwamba Allaah hana matakwa, uwezo wala kuyaumba. Tunawaraddi kwa mambo mawili:

1 – Jambo hilo linaenda kinyume na maneno Yake (Ta´ala):

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ

”Allaah ni Muumbaji wa kila jambo.”[1]

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“Allaah amekuumbeni pamoja na vile mnavovifanya.”[2]

2 – Allaah ndiye anayemiliki mbingu na ardhi. Vipi katika ufalme Wake kutakuwa yale ambayo hayahusiani na matakwa na uumbaji Wake?

[1] 39:62

[2] 37:96

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 96
  • Imechapishwa: 06/11/2022