53. Mtazamo wa Jabriyyah juu ya makadirio ya Allaah

Kuna mapote mawili yaliyoenda kinyume katika mipango na makadirio:

1 – Jabriyyah. Wanasema kuwa mja ametenzwa nguvu juu ya matendo yake na hana khiyari katika jambo hilo. Tunawaraddi kwa mambo mawili:

1 – Allaah ameyaegemeza matendo ya mtu kwake na amefanya kuwa yeye ndiye ameyachuma; anaadhibiwa na analipwa thawabu kutokana na vile atakavyotenda. Angekuwa ametenzwa nguvu basi isingesihi kumnasibishia nayo na kule kumuadhibu kwayo ingelikuwa ni dhuluma.

2 – Kila mmoja anajua tofauti kati ya kitendo ambacho mtu anakifanya kwa kutaka kwake mwenyewe na asichofanya kwa kutaka kwake inapokuja katika ule uhakika na  hukumu. Endapo mtu atamshambulia mwingine na akadai kuwa ametenzwa nguvu juu ya kufanya hivo kutokana na mipango na makadirio ya Allaah, basi kitendo hicho kingezingatiwa kuwa ni upumbavu unaoenda kinyume na yanayotambulika kilazima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 96
  • Imechapishwa: 06/11/2022