Wakeze Mtume ni katika jamaa zake

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa jamaa (الآل) ni wake na kizazi kama ilivyokuja katika upokezi wa Abu Humayd?

Jibu: Wanaingia humo. Kama alivosema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ

“Waingizeni watu wa Fir’awn katika adhabu kali kabisa.”[1]

Bi maana wafuasi wa Fir´awn. Wake na kizazi wanaingia katika jamaa. Hawaingii humo wale wasiokuwa miongoni mwao kama vile Abu Lahab, Abu Twaalib na wazazi wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa hawaingii humo, kwa sababu sio katika waumini.

[1] 40:46

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23021/هل-المقصود-بالال-الازواج-والذرية
  • Imechapishwa: 14/10/2023