Swali: Ni ipi hukumu ya kumsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba ndio jicho la ulimwengu?

Jibu: Hili ni batili. Ni maneno yasiyokuwa sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mmoja katika walimwengu. Hata hivyo yeye ndiye kiumbe bora. Kwa maneno yake hayo kama anakusudia yeye ndiye kiumbe bora ni maana sahihi. Lakini asiseme matamshi hayo. Atamke matamshi yanayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah; bwana wa wana wa Aadam na kiumbe bora – swalah na amani ziwe juu yake.

Swali: Baadhi yao wanasema:

حيّاك الله بأنوار النبي

“Allaah akupe uhai kwa nuru za Mtume.”

Jibu: Yote haya hayana mategemezi. Inatosha kumuombea kwa Allaah ampe uhai, Allaah ambariki, Allaah amfanyie wema na kwamba Allaah amtengeneze. Matamshi haya ni katika ukhurafi wa waliochupa mipaka ambao wamesheheni kwa ujinga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23011/حكم-قول-الرسول-عين-الكون-وبانوار-النبي
  • Imechapishwa: 14/10/2023