Swali: Nilivaa soksi asubuhi na nikawa nimepangusa juu yake wakati wa kutawadha kwa ajili ya kuswali Dhuhr. Ilipofika wakati wa ´Aswr nikavaa soksi nyingine juu yake. Je, inajuzu kwangu kupangusa kwenye zile soksi zilizoko juu?

Jibu: Hapana, ukianza kupangusa kwenye soksi kisha juu yake ukavaa zingine, unatakiwa kupangusa kwenye zile za kwanza ambazo ulianza kuvaa. Ukianza kupangusa juu yake na ukavaa juu yake zingine, usipanguse kwenye zile ambazo ziko juu. Unachotakiwa ni kupangusa kwenye zile za kwanza ambazo ulianza kupangusa juu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-4_1.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020