Swali: Muulizaji achague Fatwa ipi wakati ambapo Fatwa za wanachuoni zimekuwa nyingi juu ya suala fulani?

Jibu: Fataawa zinatofautiana. Fatwa ambayo imesimama juu ya dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah ndio ambayo inatendewa kazi. Kuhusiana na Fatwa ambayo dalili yake haiko wazi, hii ithibitishwe na isichukuliwe moja kwa moja ilihali dalili yake haiko wazi. Hili ni jambo la kwanza.

Jambo la pili ni kwamba, unapomuuliza mwanachuoni ambaye unaamini elimu na Dini yake usiende kuwauliza wengine. Umeshauliza na umeshajibiwa inatosheleza. Jibu lake alilokupa linatosha na usiende kuuliza wengine. Kwa kuwa utaanguka katika tofauti kati ya hawa wawili na kuchanganyikiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/adaab-11-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2015