Namna hii ndivyo elimu inavyotafutwa

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ

“Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja kwenda (kupigana vita vya jihaad). Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze (Dini).” (09:122)

Wakajifunze Dini kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa wanachuoni baada yake.

Uelewa ndio elimu. Elimu sio kuhifadhi sana, bi maana ukahifadhi vitabu vikubwa vikubwa kama al-Bukhaariy, Muslim na Sunan. Hifadhi utakavyo lakini pamoja na hivyo wewe sio mwanachuoni. Wewe ni mwenye kuhifadhi vitabu tu pasina ya kujua yaliyo ndani yake. Elimu sio kwa kuhifadhi tu kama ambavyo sio kwa kuelewa tu. Ni lazima kupatikane mambo yote mawili; kuhifadhi na kuelewa. Hifadhi na halafu uelewe uliyohifadhi. Sio wewe ndiye utajifahamisha. Kuhusu uelewa hili utalipata kupitia kwa wanachuoni. Wao ndio watakufafanulia na kukuwekea wazi. Hii ndio njia ya kujifunza. Ikiwa unataka elimu basi hii ndio njia ya kujifunza.

Hili bila ya shaka ni gumu na linahitajia kusafiri. Linahitajia vilevile mtu kuwa mgeni na kuwa mbali na familia na mji wa mtu. Lakini hata hivyo ni lazima iwe hivyo kwa mwanafunzi. Ama mtu kusema kuwa hawezi kusafiri kwa kuwa yuko na vitabu ambavyo anaweza kusoma ndani yake, mikanda anayoweza kusikiliza na marafiki anaoweza kusaidiana nao katika kuvifahamu kuvitabu. Njia zote hizi sio sahihi na hatimae zinapelekea katika ujinga na madhara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/adaab-11-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2015