Swali: Je, bora ni kuswali vipindi vitano vya swalah mwanzoni mwa wakati au mwishoni mwake?
Jibu: Bora ni kuswali swalah tano mwanzoni mwa wakati isipokuwa ´Ishaa. Kuichelewesha mpaka theluthi ya wakati ndio bora muda wa kuwa jambo hilo haliwatii uzito maamuma. Ikiwa jambo hilo linawatia zito au linawatia uzito baadhi yao, basi kuiswali mwanzoni mwa wakati. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliichelewesha ´Ishaa mpaka ukapita sehemu kubwa ya usiku. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Huu ndio wakati wake kama isingelikuwa kuwatia uzito ummah wangu.”[1]
Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaona wamekusanyika, basi anaharakisha, akiwaona wanajivuta, basi anachelewesha.”[2]
Vilevile inacheleweshwa Dhuhr wakati wa jua kali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Kukiwa na joto kali basi pateni baridi kwa swalah.”[3]
[1] Muslim.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] al-Bukhaariy (535).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/214)
- Imechapishwa: 27/04/2026
Swali: Je, bora ni kuswali vipindi vitano vya swalah mwanzoni mwa wakati au mwishoni mwake?
Jibu: Bora ni kuswali swalah tano mwanzoni mwa wakati isipokuwa ´Ishaa. Kuichelewesha mpaka theluthi ya wakati ndio bora muda wa kuwa jambo hilo haliwatii uzito maamuma. Ikiwa jambo hilo linawatia zito au linawatia uzito baadhi yao, basi kuiswali mwanzoni mwa wakati. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliichelewesha ´Ishaa mpaka ukapita sehemu kubwa ya usiku. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Huu ndio wakati wake kama isingelikuwa kuwatia uzito ummah wangu.”[1]
Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaona wamekusanyika, basi anaharakisha, akiwaona wanajivuta, basi anachelewesha.”[2]
Vilevile inacheleweshwa Dhuhr wakati wa jua kali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Kukiwa na joto kali basi pateni baridi kwa swalah.”[3]
[1] Muslim.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] al-Bukhaariy (535).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/214)
Imechapishwa: 27/04/2026
https://firqatunnajia.com/wakati-bora-wa-swalah/