ash-Sha´raaniy ameyapokea katika ”al-Miyzaan” kutoka kwa Imaam Maalik[1], ilihali an-Nawawiy amepokea kutoka kwake tofauti na hiyo, basi ichunguzwe. Na hayo ndio maoni yaliyochaguliwa na Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah, ambaye alichagua kumfuata Ibn Hazm katika suala hili. Maoni haya ya mwisho ndio pia yamenasibishwa kwa Ibraahiym an-Nakha´iy na Ibn Abiy Laylaa, kisha akasema:

”Haya ndio maoni pekee yanayojuzu, kwa sababu hakuna katika chochote miongoni mwa masimulizi kwamba twahara inabatilika kutoka katika viungo vya wudhuu´ wala kutoka katika baadhi yake kwa kumalizika muda wa kupangusa. Bali yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza tu mtu yeyote kupangusa zaidi ya tatu kwa msafiri au mchana mmoja na nyusiku zake kwa mkazi. Basi mwenye kusema kinyume na haya ameongeza katika masimulizi yale yasiyokuwemo ndani yake na amemnasibishia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yale ambayo hakusema. Mwenye kufanya hivyo kwa kukosea hakuna kitu juu yake, lakini mwenye kufanya hivyo kwa makusudi baada ya kusimama hoja juu yake, basi amefanya dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Twahara haibatilishwi isipokuwa kwa kupata hadathi. Huyu twahara yake imesihi kwa yakini na hajapata hadathi, basi yeye ni twahara. Mwenye twahara anaswali muda wa kuwa hajapata hadathi au muda wa kuwa halijaja andiko la wazi kwamba twahara yake imechenguka hata kama hajapata hadathi. Huyu ambaye muda wake wa kupangusa umemalizika hajapata hadathi wala halijaja andiko la wazi kwamba twahara yake imechenguka, si katika baadhi ya viungo vyake wala vyote. Kwa hiyo yuko na twahara na ataswali mpaka apate hadathi. Kisha atavua soksi zake za ngozi wakati huo au kitu kingine kinachofunika mguu wake na atatawadha. Kisha ataanza kuhesabu upya upangusaji kwa muda mwingine  na kadhalika.”

Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

1370-12-08

Beirut

[1] al-Miyzaan (1/150).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 27/04/2026